TIMU za mpira wa miguu na netbali za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) zimeanza vyema kampeni za kutetea mataji yao baada ya kuzibugiza bila huruma timu za Tume ya Madini na Tume ya Nguvu za Atomic jijini Tanga.
TPA ambaye ndiye mshindi wa jumla wa mashindano ya SHIMMUTA ya msimu wa 2023 wameibugiza timu ya Madini magoli 3-0 kwa upende wa mpira wa miguu, huku kwa upande wa netbal ikiibuka na ushindi wa vikapu 33-27 dhidi ya timu ya TAEC.
Katika Mchezo huo uliopigwa katika Viwanja vya Saruji nje kidogo ya mji wa Tanga ilishuhudiwa TPA ikifungua akaunti ya mabao kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo kwa goli la 'acrobatic ' lililofungwa na Ramadhani Madebe.
Goli la pili na la tatu lilifungwa na Said Jambae aliyeingia kipingi cha pili kuchukua nafasi ya Madebe ambaye alipata majeraha yaliyomlazimu kutoka.
Mashindano ya SHIMMUTA yameanza rasmi mjini Tanga ambapo TPA imeshirikisha timu za michezo yote.
Katika mashindano yaliyofanyika mwaka jana mijini Dodoma, TPA iliibuka washindi wa jumla.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED