Wadau waendelea kubuni teknolojia kuongeza ufanisi utoaji elimu

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 04:28 PM Oct 09 2024
Mkurugenzi wa Kampuni ya Shule Soft, Ephraim Swilla, akizungumzia uzinduzi wa mfumo mpya wa kulipa ada kwa kutumia namba maalum ambayo itamtambua mwanafunzi atayelipa ada, mfumo huo unatumika kwa benki na mtandao wowote wa simu na mahali popote nchini.
PICHA: GRACE MWAKALINGA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Shule Soft, Ephraim Swilla, akizungumzia uzinduzi wa mfumo mpya wa kulipa ada kwa kutumia namba maalum ambayo itamtambua mwanafunzi atayelipa ada, mfumo huo unatumika kwa benki na mtandao wowote wa simu na mahali popote nchini.

KATIKA kuboresha mifumo ya uendeshaji elimu nchini. Wadau wameendelea kubuni teknolojia zinazosaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu na kurahisisha upatikanaji wa maarifa.

Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na Kampuni ya Shule Soft, inayojihusisha na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa shule nchini ambao wamejikita katika kuhifadhi na kusimamia taarifa zote za wanafunzi, ikiwa ni pamoja na taarifa za usajili, mahudhurio, na maendeleo ya kitaaluma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shule Soft, Ephraim Swilla, Octoba 8, 2024, amezindua mfumo  mpya wa  namna wazazi au walezi watalipa ada kwa namba maalum ambayo itamtambua mwanafunzi aliyelipiwa.

Amesema mfumo huo umeanzishwa ili kutatua changamoto ya baadhi ya shule kushindwa kupata risiti au taarifa za wanafunzi waliolipa ada na matokeo yake ni watoto kurudishwa nyumbani na wakati mwingine kushindwa kufanya mitihani.
 
Alisema mfumo huo, unatoa nafasi kwa wazazi au walezi kulipa ada kwa kutumia benki au mtandao wowote wa simu, kulingana na mazingira alipo na  fedha hiyo itaingia moja kwa moja kwenye mfumo wa shule.

“Mfumo huu ni maalum kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya fedha kutoonekana kwenye mifumo na matokeo yake wazazi kuendelea kudaiwa, tumekuja na suluhisho hili, ambalo litasaidia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji ada na kuondoa malalamiko kwani itamtambua nimwanafunzi yupi amelipa,” amesema Swilla.

Mkuu wa masoko kutoka Selcom, Shumbana Walwa akizungumzia faida za mfumo huo akidai utaondoaa usumbufu wa wanafunzi kurudishwa nyumbani au kushindwa kufanya mitihani wakidaiwa hawajalipa ada.

Ameongeza kuwa mfumo huo mpya hauna makato yeyote na utazinufaisha shule zaidi ya 450 zilizoko mikoa mbalimbali nchini, ambazo ni za msingi, sekondari na vyuo vya kati.

Amesema mfumo huo umeunganishwa kati ya mtoa huduma na mteja, kwa shule watapata  ujumbe mfumo wa maneno( sms) pamoja na barua pepe, aliongeza kuwa kampuni inahudumia zaidi shule binafsi huku za serikali zikiwa ni saba tu.

Mkuu wa Masoko kutoka Selcom, Shumbana Walwa, amesema mifumo mingi ya ulipaji ada inakabiliwa na changamoto ikiwemo fedha kutoonekana kwenye mfumo, uzinduzi wa hatua hiyo ni rahisi na utasaidia kufahamu malipo yaliyofanyika.

Alisema zipo faida za kutumia mfumo huo ikiwamo kumuweza mwanafunzi kusoma kwa utulivu badala ya kusumbuliwa kwa sababu ya mifumo isiyosomana.

Amezihamasisha shule na wazazi kujiunga na mfumo huo kutumia mfumo huo kulipa ada na kwamba huduma inapatikana mikoa mbalimbali ikiwamo Mbeya, Arusha, Tabora, Dar es Saalam, Geita.

Mkuu wa biashara kutoka Kampuni ya Shule Shule Soft, Elisha Tengeni, amesema ulipaji wa kidigitali unasaidia kubaini waliolipa ada katika muda uliopangwa, aliomba shule kujiunga na mfumo huo ili kuepuka malalamiko na upotevu wa fedha kwenye  baadhi ya mifumo.
Picha ya pamoja.