Tuzo za rais kuchochea uwajibikaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:26 PM Nov 11 2024
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exhaud Kigahe (wapili kulia) akikabidhi tuzo kwa muwakilishi wa Kampuni ya Bima za Maisha ya Jubilee kama moja ya watoa huduma bora za kijamii.
Picha Mpigapicha wetu.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exhaud Kigahe (wapili kulia) akikabidhi tuzo kwa muwakilishi wa Kampuni ya Bima za Maisha ya Jubilee kama moja ya watoa huduma bora za kijamii.

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exhaud Kigahe ameipatia tuzo Kampuni ya Bima za Maisha ya Jubilee kama ishara ya kutambua mchango wake katika ufanisi wa huduma ambazo zinaleta matokeo chanya kwa jamii, huku ikielezwa kuwa tuzo hizo zitasaidia kuchochea uwajibikaji.

Waziri Kigahe aliipatia kampuni hiyo tuzo hiyo mwishoni mwa juma katika hafla ya utoaji Tuzo za Rais iliyofanyika mkoani Dar es Salaam ambako Makamu wa Rais wa Philip Mpango alihudhuria kama mgeni rasmi.

Sehemu ya taalifa iliyotolewa na kampuni hiyo, iliahidi kuendelea kujitoa kwaajili ya kusaidia uhakika wa usalama wa maisha kwa watu wa hali ya chini na watanzania kwa ujumla.

"Jubilee inayofuraha kwa kupokea tuzo hii ya 'President's Manufacturer of The Year Awards 2024' katika kipengele cha mtoa huduma bora na inaahidi kuendelea kutoa huduma zenye ufanisi kwa Watanzania ili kusaidia katika kulinda ndoto zao pamoja na wapendwa wao," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

1