NEMC, Ofisi ya RC DAR wasafisha mazingira

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:10 AM Jan 12 2025
NEMC, Ofisi ya RC DAR wasafisha mazingira.
Picha: Mpigapicha Wetu
NEMC, Ofisi ya RC DAR wasafisha mazingira.

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, wameshiriki kusafisha mazingira ns urejelezaji takataka katika Wilaya ya Ilala.

NEMC imeshiriki zoezi hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhamasisha wananchi kusafisha na kutunza mazingira katika maeneo yao.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa mwenyewe, Albert Chalamila aliyeambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama , Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji, pamoja na watumishi wa mkoa na Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuna umuhimu wa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji na utunzaji taka katika maeneo maalumu ili kutengeneza mbolea na nishati, jambo litakaloongeza fursa za ajira pamoja na usafi wa mazingira ili Jiji la Dar es Salaam liendee kuwa safi na kivutio kwa uwekezaji na utalii.

Washiriki wengine wa zoezi hilo ni pamoja na DAWASA, TANESCO na wafanyabiashara wa maeneo ya Wilaya ya Ilala.