Mwamposa ampongeza Lugumi kujenga maghorofa ya watoto yatima

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:24 AM Jan 12 2025
Mtume Boniface Mwamposa.

Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' wa Kanisa la Inuka Uangaze amempongeza mfanyabiashara Said Lugumi kwa kujenga maghorofa matano kwa ajili ya watoto yatima.

M“Ninampongeza Lugumi, ni jambo jema lenye roho ya kumcha Mungu,” alisema Mwamposa.

Majengo hayo, yanayotarajiwa kukamilika Machi mwaka huu, yatanufaisha zaidi ya watoto 800 wenye mahitaji maalum jijini Dar es Salaam. Awali, jengo moja la ghorofa nne lilikabidhiwa watoto hao Desemba 25, mwaka jana, wakati wa hafla ya chakula iliyoandaliwa na Lugumi.

Kila jengo lina uwezo wa kuchukua zaidi ya watoto 100.