Sensa ya watu na makazi yam waka 2022 inaonesha kuwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 watu 2,090,691 wenye umri kuanzia miaka 15 ndio waliofanikiwa kuingia katika mfumo rasmi wa ajira nchini.
Nipashe DigitalData leo kupitia Tafiti Jumuishi za Nguvu Kazi (ILFS) na Makadirio yake uliotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu tunakusogezea karibu mwenendo watu hao kuingia katika mfumo wa ajira kwa kila mwaka.
Utafiti huu unabainisha kuwa mwaka 2018 waajiriwa walikuwa 21,984,534, mwaka 2019 waliongezeka na kufikia 22,451,545 sawa na ongezeko la watu 467,011.
Kadhalika mwaka 2020 waliongezeka hadi kufikia 23,029,954 sawa na ongezeko la watu 578,409, mwaka 2021 walifikia 23,536,135 sawa na ongezeko la watu 506,181.
Aidha mwaka 2022 walipanda na kufikia 24,075,225 sawa na ongezeko la watu 539,090 ambako takwimu hizi ni kwa upande wa Tanzania Bara pekee.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED