Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk. Suleiman Jafo (wapili kulia), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge (wakwanza kushoto), na baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Tano ya Viwanda na Uwekezaji Pwani, kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Dk. Jafo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, pamoja na mambo mengine amewahimiza wenye viwanda kutambua umhimu wa kujiunga na WCF ili kulinda nguvu kazi ya wafanyakazi.
Aidha, Dk. Jafo amesifu juhudi za uongozi wa Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha mazingira rafiki kwa wawekezaji, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta ya viwanda mkoani humo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED