Mbowe: Chukueni fomu bila chuki, walionikanyaga nimewasamehe

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 05:43 PM Dec 18 2024
FREEMAN Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa).
Picha:Nipashe Digital
FREEMAN Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa).

FREEMAN Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa), amewataka wanachama wa chama hicho wanaowania nafasi tofauti za uongozi, kuchukua fomu bila chuki.

“Chukueni fomu kwa sababu ya kuwania nafasi na si kwa chuki, kulipa kisasi, hii ndio maana ya ‘No Hate No Fear’, tusiwape maadui nafasi Chadema yetu ni ya muhimu.

“Kilindeni chama kafanyeni kampeni za kistaarabu wagombea, wanachama, tusitafute mifano ya biblia ya Mfalme Suleiman kwamba ‘mtoto huyu kamkate katikati’ lazima tumwache mtoto akiwa mzima, msiwakanyage wenzenu.

“Nawatangazia mapema walionikanyaga, kuwasamehe, walionitukana nawatangazia msamaha, kwa heshima ya wanaonipenda.”

Mbowe, amesema baada ya kuombwa na wanachama wa chama hicho, kuwania tena nafasi ya uenyekiti taifa, ametoa saa 48 kutoa majibu.