Uzinduzi SGR mtaji unaomng’arisha Rais Samia nje, ndani ya mipaka

By Peter Orwa , Nipashe
Published at 02:27 PM Aug 02 2024
· Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akinadi uchumi wake nchini Norway.

TANGU aingie madarakani, leo akihesabu safari zake kusonga miaka mitatu na nusu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amekuwa na staili mbalimbali za kuboresha uchumi na biashara katika zama za awamu ya sita.

Staili hiyo inabebwa na kunadi uchumi wa kuuza kilichomo sokoni Tanzania. Mathalani, alipoanza na tamthilia ya kuuza bidhaa utalii, pia anahamasisha uzalishaji na kukaribisha wawekezaj ambao ni muhimu kuwezesha kwa mitaji, teknolojia na hata masoko. 

Ili kunakishi mikakati yake hiyo, mara moja akajitosa katika vita na ushawishi wa siasa uchumi kung’arisha nchi kwa marafiki wa uwekezaji mitaji ya kimataifa. 

Pia, hapo ndipo ukawa mwanzo wa kushuhudiwa mengi yanayotafsiriwa kama maridhiano ya kisiasa na kufunguliwa vizimba vya mikutano ya kisiasa kitaifa. 

Lingine ni kwamba, amekuwa akipambana tangu mwanzo wa utawala wake akiwekeza katika mitaji yake mikuu inayowezesha uchumi, miradi mikubwa ikiwamo Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na reli kipenzi cha Watanzania SGR na kulitekeleza hilo jana amezindua SGR. 

Ili kufanikisha malengo yake katika mazingira ya dunia ambayo sasa ina sura ya kijiji, Rais amekuwa akizuru katika mataifa tofauti akitumia ushawishi kunasa vile ambavyo uwezo wake haumo nchini.  

Baadhi ya matunda sasa yanaonekana katika nyendo kama uwekezaji ikiwamo katika sekta kama kilimo, mitaji na hata masoko ya bidhaa zake kama kunavyoshuhudiwa katika mazao ufuta na rasilimali mbolea, huku nyumbani rasilimali vijana ikiingizwa shambani kupata ajira katika teknolojia ya kisasa. 

Nyumbani nako kunatumika msukumo uliopata kampeni za kiuchumi mwaka1964 maarufu “It Can Be Done, Play Your Part’ kwa maana “inawezekana, timiza wajibu wako’ kila sekta ilipambaniwa kufikia hatua zaidi ya maendeleo. 

Ikirejewa katika ziara yake nchini Norway, Februari mwaka huu, mkuu huyo wa nchi anayeingia katika rekodi ya Rais wanawake duniani, akaitamkia hadhira iliyosika hotuba yake kwamba, mwaka huu Shirika la Fedha Duniani (IMF), limesema “Tanzania inatarajia kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani.”  

Rais Dk. Samia akibeba ajenda yake ya ushawishi mitaji, fursa za masoko na uzalishaji kuegemea nchini kwake, akawataka wawekezaji wa Norway kuja nchini Tanzania, kwani kuna mazingira mazuri ya kisiasa, kijiografia na kiuchumi. 

Iikuwa jijini Olso, akihutubia mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili, Rais Samia akabainisha kwamba tayari zipo kampuni kadhaa za Norway zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.

Aidha, Dk.Samia akawaambia kwamba:“Tanzania ina amani chini ya demokrasia imara ya mfumo wa vyama vingi, unaozingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.”

Ni hoja ambayo akaiunganisha na faida za kijiografia, akiwashawishi wawekzaji wa nchi hiyo na wengineo kuchagua Tanzania kuwekeza, kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa manane ya Afrika inayopakana nayo.

Hata hivyo, bado tunu ya bandari ina muskatakabali mpana, hadi sasa kukiwapo nyingine baharini Mtwara, Tanga na bandari ndogo Bagamoyo, pia nyingine nyingi za katika maziwa mbalimbali nchini zikiendelea kufanyiwa maboresho makubwa.

Rais akatetea sera za uchumi wa nchi kwamba, ni imara na huku ukuaji wa pato la taifa (GDP) kwa sasa likiongezeka kwa kasi nzuri, asilimia 5.2 kwa mwaka, kukiwapo matarajio kufika aslimia sita kipindi kijacho, baada ya kuondokana na misukosuko ya maradhi ya COVID 19 duniani.

Rais Dk. Samia, akawasistiza wawekezaji wa Norway na serikali yao, kwamba kuna fursa tano za kupewa kipaumbele, akizitaja kuwa ni: kilimo, nishati mbadala, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na usafirishaji.

Ni aina ya uwekezaji ambao Rais Dk. Samia kwa kuzungika na maudhui kama hayo, amekuwa akisambaza hoja yake katika nchi mbalimbali duniani, ziungane kitaifa kukuza uchumi unaopiganiwa sasa na serikali.

SGR, BWAWA NYERERE

 Mbali na kuwapo mazingira wezeshi ya kwa kunufaisha siasa uchumi, miradi miwili mikubwa ya kiatifa inayotelezwa sasa, ina tafsiri pana katika kasi ya ukuaji uchumi wa nchi na ushawishi wa uwekezaji kimataifa, ikiunganishwa na pacha wao bandari za  nchini.

Msingi wa rasilimali nishati inavyojitosheleza kitaifa, daima inatoa tafsiri pana katika hatua ya uchumi wa nchi, samambaba na ‘binamu yake’ miundombinu ya usafiri.

Ikianzia na mvuto katika Afrika Mshariki, mathalan maboresho ya bandari iiyoko mkoani Rukwa na barabara zake, tayari imeleta mvuto mkubwa na soko bandari ya Dar es Salama, ambayo sasa inaunganishwa moja kwa moja na nchi jirani kama Zambia, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Congo (DRC).

Hatua ya kizinduliwa usafiri wa treni kwa reli ya SGR, pia mtambo mwingine wa umeme katika Bwawa la Umeme a Mwalimu Nyerere, kuwashwa hivi karibuni, kunabeba maana kubwa katika maendeleo ya uwekezaji wa ‘Tanzania mpya yenye uchumi unaokua wa kasi’ kwa wa mujibu wa IMF.

Tafasiri hiyo kiuchumi na siasa, inachangia kasi ya uchumi kuua kwa kasi nchini na kimataifa,uchumi unang’ara kukaribisha mitaji ya mbali, kama alikokuwa nchini  Norway.

Ni changamoto sasa kwa watendaji wa kiserikali kuendelea alikoishia Rais katika jitihada zake, katika kukamilisha maendeleo ya uchumi wa taifa.

Simulizi ya maboresho  ya kimfumo na kimtaji inapaswa kufungua nja zaidi, mathalani viwanda vipya vinavyowekezwa kuwa chanzo cha hatua zaidi.


 
 

·       Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akinadi  uchumi wake nchini Norway. PICHA: IKULU