WATU 11 wamepoteza maisha usiku wa kuamkia leo katika ajali ya barabarani, baada ya kugongwa na lori lililokuwa limebeba saruji, kupoteza mwelekeo na kuwagonga watu hao waliokuwa wakishangaa ajali nyingine ya gari dogo aiana ya Tata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani, ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Chang’ombe kilichopo Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni.
Akizungumza na Nipashe leo, Januari 14, 2025, amesema watu hao waliopoteza maisha, walikwenda eneo la ajali hiyo wakilenga pamoja na mambo mengine kutoa msaada, baada ya kutokea ajali ya gari dogo aina ya Tata na ndipo walipokumbana na umauti.
Balozi Dk. Buriani, amesema ajali hiyo pia, licha ya kusababisha vifo 11 na kuachja wengine 11 wakiwa majeruhi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED