MWENYEKITI wa Mtaa wa Saranga, uliopo Ubungo,Dar es Salaam Leonard Mbangile, amepokelewa kwa kukabidhiwa kero kadhaa zinaowasumbua wakazi wa mtaa huo, ikiwamo ubovu wa barabara, kukosekana kwa maji na ulinzi na usalama.
Vilevile, kulipishwa ankara ya maji kutokana na hewa zinazofuka kwenye mabomba ya maji yasiyotoka.
Mbangile aliitisha mkutano wa kuwashukuru wananachi kwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, ambapo yeye ndiye aliyeshinda, hivyo akatangaza vipaumbele vilivyopo chini ya uongozi wake, ambapo ameahidi kuendelea kutatua kero kadhaa.
Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati katika mtaa huo, kwa kufatilia fedha manispaa ili iweze ikiwezekana kukamilika mwaka huu ianze huduma, hatua hiyo iyawaondolea kero wajawazito kupimwa ndani ya ofisi ya Mwenyekiti watoto kupimwa uzito chini ya mti mkubwa nje ya ofisi hiyo.
Baada ya kuzungumza hayo na mengine kadhaa akawaruhusu wanachi kuuliza maswali na kutoa maoni au ushauri. Licha ya kumpongeza kwa ushindi wengi kati ya waliopewa nafasi hiyo, walielezea jinsi ambavyo kumekuwa na ucheleshwaji wa utetekeleza wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege ahadi iliyopaswa kuanzi kutekelezwa Septemba 2024.
Dickson Malangala alilalamika kwamba baadhi ya watu wamefungiwa mabomba lakini hayatoi maji kama walivyotarajia, hivyo inawapa wakati mgumu na hasa wanapopelekewa bili, ambazo zinaonyesha matumizi ya maji.
Mkazi mwingine maarufu kwa jina la Bibi Mngoni alimweleza mwenyekiti huyo jinsi ambavyo wamekuwa na wakati mgumu wa kushuhudia wakazi wenzao wenye uwezo wa kufunga mota wakifanikiwa kupata maji na kuzaja kwenye maboza lakini wao mabomba hayatoi maji kwa kuwa presha ni ndogo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED