Bolt yatahadharisha safari za nje ya mtandao kwa madereva na abiria wakati wa sikukuu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:45 AM Dec 23 2024
Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu Bolt Tanzania.
Picha: Mtandao
Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu Bolt Tanzania.

Jukwaa linaloongoza kwa huduma ya usafiri nchini Tanzania Bolt, limetoa tahadhari kali kwa abiria na madereva kujiepusha na safari za nje ya mtandao.

Tahadhari hiyo inakuja kama sehemu ya dhamira inayoendelea ya Bolt ya kuhakikisha usalama wa abiria na madereva kwenye jukwaa lake.

Usafiri unaopangwa nje ya mtandao wa Bolt uhatarisha usalama mkubwa kwa madereva na abiria, pia utakuwa unakwepa hatua za usalama za ndani ya mtandao wa Bolt, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa safari, uthibitishaji wa utambulisho na mifumo ya usaidizi wa dharura.

Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu Bolt Tanzania alisisitiza umuhimu wa kuzingatia mifumo ya mtandao wa Bolt kwa abiria wote "Kwa Bolt, usalama ni kipaumbele chetu cha juu. Safari za nje ya mtandao hudhoofisha vitengo vya usalama tulivyonavyo ili kulinda watumiaji wetu, kama vile ukaguzi wa magari, ufikiaji wa taarifa za dharura na kujua mahali ulipo kwa wapendwa wako ukiwa safarini. 

Tunawashauri sana madereva na abiria wetu kutumia programu ya Bolt kwa safari zao zote ili kuhakikisha usalama wao. Kwa kuweka safari ndani ya mifumo yetu ya mtandao, watumiaji wanahakikishiwa usalama ambao mfumo wetu hutoa."

Vitengo vya usalama vya ndani ya programu ya Bolt ni pamoja na:
● Shirikisha Eneo Ulipo: Abiria na madereva wanaweza kushirikisha mahali walipo kwa wakati halisi na maelezo ya safari—kama vile kuchagua gari, muundo, nambari ya usajili na kujua eneo ulipo kwa salama kwa kutumia kiongoza safari.

● Usaidizi wa Dharura: Katika hali ya dharura, abiria na madereva wanaweza kutahadharisha timu ya kushughulikia dharura kwa haraka na kwa uangalifu kwa kutumia kitufe cha Usaidizi wa Dharura wa ndani ya programu. Kipengele hiki pia huarifu timu ya usalama ya Bolt, ambayo itapiga simu ya haraka ili kuhakikisha hali hiyo inashughulikiwa mara moja.

● Kukagua Safari: Timu ya usalama ya Bolt hufuatilia safari kwa makini ili kugundua jambo lolote lisilo la kawaida wakati wa safari, na kuhakikisha kwamba itashughulikia suala lolote kwa wakati linapohitajika.

● Msaada wa Usalama kwa muda wote: Timu yetu ya usalama iliyojitolea inapatikana kila saa ili kutoa msaada  wakati wa safari na baada ya safari.
Abiria wanahimizwa kuripoti tabia yoyote ya kutiliwa shaka au isiyofaa kupitia program zetu kwa uchunguzi wa haraka. Bolt inasalia na nia ya kutengeneza hali salama na ya kuaminika isiyo na mashaka ya usafiri kwa watumiaji wote nchini Tanzania.

Kampuni itaendelea kuwekeza katika vitengo vya usalama na kampeni za uhamasishaji kwa umma kushughulikia masuala ya usalama katika sekta ya usafirishaji.