WANAFUNZI saba wa Shule ya Msingi Ghati Memorial wanahofiwa kufariki dunia baada ya gari la shule waliokuwemo kuangukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo, Kata ya Muriet mkoani Arusha.
Korongo hilo lililojaa maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku usiku wa kuamkia leo Aprili 12, 2024, ilisababisha maji kufurika kwenye mto huo na barabarani.
Wakizungumza katika eneo la tukio,mashuhuda wamesema kuwa saa 12 asubuhi, gari lenye namba za usajili T 496 EFK lilikatiza juu ya barabara hiyo, dereva alishindwa kulidhibiti, hivyo liliyumba kabla ya kuangukia katika korongo hilo linalomwaga maji yake katika mto mkubwa wa Themi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED