Barabara ya Jangwani yafungwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:04 PM May 09 2024
Barabara ya Jangwani.
Picha: Mpigapicha Wetu
Barabara ya Jangwani.

BARABARA ya Jangwani jijini Dar es Salaam, imefungwa baada ya kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini huku safari za mabasi yaendayo kasi kutoka Kimara kuelekea Kivukoni na Gerezani yakiishia Magomeni Mapipa.

Aidha, mabasi yanayofanya safari zake katika maeneo ya mjini, Muhimbili na Gerezani yataendelea kufanya safari zake pamoja na Kimara hadi Morocco kwani barabara zake hazina changamoto.

Maeneo mbalimbali mjini yameendelea kuwa na foleni kubwa kutokana magari mengi kutumia njia moja baada ya njia ya Jangwani kufungwa.