Tembo wavamia makazi ya watu na kuharibu nyumba za wananchi Ikungi

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 08:33 PM Oct 26 2024
Tembo
Picha:Mtandao
Tembo

TEMBO wamevamia kata za Mkiwa na Isuna katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kufanya uharibifu mkubwa wa makazi ya watu.

Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, amemweleza hayo leo Oktoba 26, 2024 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa,wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku tano katika Mkoa wa Singida ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Mtaturu amesema tembo hao baada ya kuvamia vijiji vya kata hizo wameharibu nyumba za kaya nane na kwamba Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya imefika katika kata hizo kujionea uharibifu ukiofanywa na tembo hao.

Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu.