Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amekemea tabia ya baadhi ya waajiri kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi.
Akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Rasilimaliwatu na Utawala katika utumishi wa umma kutoka kwenye Wizara, Wakala, Mamlaka, Mashirika na Taasisi za serikali, jana jijini hapa, Waziri Simbachawene amesema waajiri hao wamekuwa hawawapokei, kukataa na kuficha barua zenye maelekezo mahsusi ikiwamo barua za uhamisho (kuhamia na kuhama).
“Ninyi mliopo humu ndio washauri wakuu wa waajiri wenu, haya yanayofanyika ni kinyume cha utaratibu na ni utovu wa nidhamu, na halivumiliki endapo kweli tunataka kujenga utumishi wa umma na hapa nitoe melekezo kwa utaratibu huu mpya uachwe kwa kuwa kinachofanyika ni kinyume na utaratibu,”amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED