RC Simiyu awaongoza wananchi kumuombea Rais Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:56 PM Dec 23 2024
RC Simiyu awaongoza wananchi kumuombea Rais Samia
Picha:Mpigapicha Wetu
RC Simiyu awaongoza wananchi kumuombea Rais Samia

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi amewaongoza viongozi na wananchi mbalimbali mkoani humo kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuendelea kuwa imara katika kuliongoza taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya kiongozi huyo, maombi hayo yamefanyika leo mkoani Simiyu sambamba na matembezi, yaliyolenga kuhamasisha udumishaji wa amani na utulivu kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

"Mbali na kumuombea Rais, maelfu ya wananchi walitumia nafasi hiyo kuliombea taifa kuvuka salama mwaka 2024 na kuingia 2025 likiwa na umoja, wenye amani na mshikamano," imesema sehemu ya taarifa hiyo.