Lissu atangaza nia kuwania urais 2025

By Enock Charles , Nipashe
Published at 07:46 PM Jul 26 2024
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu.
Picha: Enock Charles
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu ametangaza nia kuwania nafasi ya urais mwakani na kwamba chama chake kinajiandaa kupata ushindi wa kutosha dhidi ya Rais Samia Suluhu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye anatarajiwa kugombea kupitia chama hicho.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya kurejea kutoka nje ya nchi alipokuwa kwa mapumziko mafupi baada ya ziara ya chama chake Kanda ya Kaskazini aliyoifanya sambamba na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Lissu alisema kwa sasa chama chake kinaandaa wagombea katika nafasi mbalimbali kwa ajili ya kushinda uchaguzi ujao.
 
“Nia yangu ya kugombea mwaka 2025 iko palepale nitaitikia wito Watanzania na nitaitikia wito wa chama changu” amesema Lissu.
 
Alipoulizwa kuhusu kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chake amesema hana mpango huo na kukanusha uvumi wakuwepo mgogoro kati yake na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe  kuhusu kuwania nafasi hiyo.
 
“Nimesema mara mia kwamba sigombei uenyekiti wa chama sasa huo mvutano unatoka wapi ni wa kutengenezwa tu na vyombo vya habari” amesema Lissu.