Hatima ya Mwabukusi TLS kesho

By Restuta James , Nipashe
Published at 04:41 PM Jul 25 2024
 Wakili Boniface Mwabukusi.
Picha: Mtandao
Wakili Boniface Mwabukusi.

Hukumu ya kesi hiyo kati ya Mwabukusi dhidi ya TLS, ipo Mahakama Kuu (Masijara Ndogo ya Dar es Salaam), mbele ya Jaji Butamo Kasuka Phillip.

Hukumu ya kesi ya kupinga kuenguliwa kuwania urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), iliyofunguliwa na Wakili Boniface Mwabukusi, imepangwa kutolewa kesho Julai 26, 2024 kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Hukumu ya kesi hiyo kati ya Mwabukusi dhidi ya TLS, ipo  Mahakama Kuu (Masijara Ndogo ya Dar es Salaam), mbele ya Jaji Butamo Kasuka Phillip.

Taarifa ya mawakili inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imewataka mawakili wote kujitokeza kumsindikiza Mwabukusi.

Mawakili wote wapenda haki tujitokeze kwa idadi kubwa sana kuhudhuria hii kesi ya Mwabukusi Vs Tanganyika Law Society, ambayo imebeba maslahi mapana ya Mawakili na Wananchi wa Tanzania." imesema sehemu ya taarifa hiyo.