CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Amos Makalla, marehemu alikuwa anajiandaa kuhudhuria semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.
"Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kutokana na kifo cha ghafla na cha kikatili.
"Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria," amesema Makalla.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED