TAASISI ya Jubilee Life Insurance imeshinda tena tuzo zitolewazo na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kama kampuni ya bima za maisha zilizowasilisha vizuri taarifa zake za fedha kwa mwaka 2023 ikishika nafasi ya kwanza kipengele cha bima nchini.
Akizungumza leo baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Helena Mzena, ameipongeza timu nzima ya Jubilee Life kwa kazi nzuri wanayoifanya, huku akiishukuru bodi hiyo kwa kuona mchango wao mzuri katika uwasilishaji wa taarifa zake za fedha.
"Pia tunawaahidi watanzania kuendelea kuwapatia huduma bora za bima za maisha, pamoja na kuhakikisha kwamb kunakuwa na usahihi zaidi katika uwasilishaji wa taarifa zetu za fedha," amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED