Akamatwa Mloganzila akichangisha fedha za msaada

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 03:56 PM Dec 04 2024
Kija Mayunga
Picha: MNH-Mloganzila
Kija Mayunga

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, imemkamata mtu aliyefahamika kwa jina la Kija Mayunga, akidaiwa kuwatapeli ndugu wa wagonjwa kwa madai ya kuwasaidia, ili wapate huduma.

Mayunga amekamatwa leo akiwa eneo la hospitali hiyo, akifanya tukio hilo na tayari amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni, kilichopo Kibamba, wilaya ya Ubungo, es Salaam, kwa hatua zaidi.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano hospitalini hapo, ilisema uongozi wa MNH-Mloganzila, ilitoa wito kwa wananchi kufuata utaratibu wa kupata huduma, ikiwamo utaratibu wa malipo uliowekwa kuepuka matapeli.