WAKATI siku 16 za uanaharakati kupinga ukatili zikiwa zimeingia juma la pili, wanafunzi wa shule mbili shikizi za msingi za Azimio na Papiliki zilizoko Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi, wameeleza namna wanavyochukizwa na matukio ya ukatili wa kingono, hasa ubakaji na ulawiti yanavyojitokeza kila uchao, licha ya adhabu kali inayotolewa na mahakama.
Wakizungumza leo katika kongamano la elimu ya ukatili lililofanyika viwanja shule hizo katika Kijiji cha Uchira, baadhi ya wanafunzi hao akiwamo (jina limehifadhiwa), amesema yeye ni miongoni mwa watoto aliyeshuhudia mwenzake aliyekuwa akiishi nae alivyopoteza ndoto yake, baada ya kubakwa nyumbani kwao.
Mwanafunzi mwingine, (jina limehifadhiwa), amesema wamepata faraja ya kuwaona wanaharakati walivyoamua kuwafikia na kuwafumbua macho kuhusu ukatili unaofanyika dhidi yao na kulifanya kundi hilo kuwa miongoni mwa makundi yanayoathiriwa zaidi.
Kongamano hilo la elimu ya ukatili, limeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la KWIECO, linalofanya kazi hiyo na wanaharakati kutoka Jukwaa la Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi (TAPO) pamoja na Wasaidizi wa Kisheria....
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED