REA yatoa mitungi ya gesi yenye ruzuku 19,530 Singida

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 03:49 PM Dec 04 2024
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego.
Picha: Mtandao
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego.

KATIKA kuziwezesha kaya za vijijini na mijini kuhakikisha zinatumia nishati safi ya kupikia serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itatoa mitungi ya gesi 19,530 yenye ruzuku kwa Mkoa wa Singida ambayo itauzwa kwa bei ya chini ya Sh.20,000 kwa mtungi mmoja.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, akizungumza leo (Disemba 4, 2024) baada kupokea maafisa kutoka REA ambao wameleta mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi yenye ruzuku, alisema mitungi hiyo itagawiwa kwa uwiano sawa katika wilaya zote tano za Mkoa wa Singida.

Naye Mhandisi Mwandamizi kutoka REA,Deusdedit Malulu, amesema mradi wa kusambaza mitungi ya gesi yenye ruzuku kwa mkoa wa Singida itaanza kutekelezwa Januari 2025 ambayo itakuwa na ujazo wa kilo sita ambapo kwa  nchi nzima mitungi 452,000.