Waandamanaji Kenya waapa kurudi tena barabarani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:43 PM Jun 26 2024
Waandamanaji nchini Kenya waapa kurudi tena barabarani kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Picha: Gerald Anderson/Anadolu/picture alliance
Waandamanaji nchini Kenya waapa kurudi tena barabarani kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024.

WAANDAMANAJI nchini Kenya wameapa kuendelea na maandamano yao kupinga nyongeza mpya za ushuru, siku moja tu baada ya polisi kufyatua risasi na kuua takriban watu watano na kujeruhi zaidi ya watu 100.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema amesikitishwa na ripoti za mauaji na majeruhi zilizotokea katika purukushani za kupinga mswada huo tete wa fedha wa mwaka 2024.

Guterres ameitaka serikali kuwa na uvumilivu kwa watu wake na kuwaruhusu kuandamana kwa amani. 

Wafuasi wa vuguvugu la maandamano hayo yaliyopewa jina la “siku saba za hasira” wametumia mitandao ya kijamii kuelezea dhamira yao ya kurudi tena barabarani siku ya Alhamisi.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, wametumia hashtag ya Tukutane Alhamisi.

DW