Waziri Mkuu ataka wafanyabiashara wasikilizwe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:57 PM Jun 28 2024
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Picha: Maktaba
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameziagiza Mamlaka zote za Serikali kusimamia na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara Nchini na kuzitaka Mamlaka hizo kushirikiana na Serikali ili kutatua kero na changamoto za Wafanyabiashara Nchini.

Majaliwa ametoa maelekezo hayo wakati akisoma hotuba ya kuahirisha shughuli za Bunge la Bajeti kwa mwaka 2024/25 ambalo limeketi kwa takribani miezi mitatu Jijini Dodoma.

“Wafanyabiashara wasikilizwe na kuona namna bora ya utatuzi wa changamoto zinapojitokeza, Serikali itaendelea kuwapokea na kuwasikiliza Wafanyabiashara na mchango wao katika kukuza uchumi wa Nchi yetu niwahakikishie Wafanyabiashara wote kuwa Serikali inahakikisha wanafanya shughuli zao kwa mafanikio”