Kadhaa wakamatwa kuhusika na shambulizi la Moscow

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:03 AM Apr 02 2024
Mshukiwa wa shambulizi la kigaidi la mjini Moscow afikishwa mahakamani.
Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/dpa/picture alliance
Mshukiwa wa shambulizi la kigaidi la mjini Moscow afikishwa mahakamani.

IDARA ya Usalama ya Urusi FSB, inawashikilia watu kadhaa ambao wanashukiwa kuhusika na shambulizi la kigaidi kwenye ukumbi wa tamasha wa Crocus Kaskazini-Magharibi mwa Moscow zaidi ya wiki moja iliyopita.

FSB imesema kuwa raia wanne wa kigeni ambao walihusika moja kwa moja katika ufadhili na kuwapa vifaa magaidi, wamezuiliwa mjini Dagestan katika eneo la Urusi la Caucasus ya Kaskazini.

Vyombo vya habari vya serikali vimeonesha video iliyotolewa na FSB ambapo mwanamume ambaye hakutambulishwa anasema aliwapa silaha wahalifu hao kwenye mji mkuu wa Dagestani, Makhachkala kufanya mashambulizi hayo katika ukumbi wa Crocus.  

Hata hivyo, video hiyo haikuweza kuthibitishwa. Washukiwa wengi pia wamekamatwa nchini Tajikistan.