Tigo yashinda tena tuzo ya Ookla

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 06:22 PM Oct 23 2024
Tigo yashinda tena tuzo ya Ookla
Picha:Mtandao
Tigo yashinda tena tuzo ya Ookla

KAMPUNI ya simu ya Tigo kwa mara ya pili mfululizo imeshinda imeshinda Tuzo ya kimataifa ya Ookla (Speedtest Award 2024) kwa kuwa Mtandao wenye Intaneti yenye kasi zaidi Tanzania.

Tuzo za 'Speedtest Awards' hutolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Ookla iliyopo Marekani ambayo inahusika na upimaji wa ubora wa huduma na utendaji kazi wa mitandao mbalimbali ya simu duniani ambapo hutoa tuzo kwa mitandao inayofanya vizuri. 

Kwa mwaka jana, kampuni hiyo ya simu ilishinda pia tuzo hiyo na kufanya mwaka huu wakiwa wanatimiza miaka 30 ya kutoa huduma hapa nchini, kushinda kwa mara ya pili mfululizo.

Speedtest Awards.