Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, leo tarehe 23 Oktoba 2024, ametembelea Maonesho ya Kongamano la 10 la Jotoardhi yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Akiwa katika maonesho hayo, Dk. Mpango alikutana na Kaimu Mkurugenzi wa Umeme kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mha. Aurea Bigirwamungu katika banda la mamlaka hiyo.
Wakati wa mazungumzo yao, Mha. Bigirwamungu amemweleza Makamu wa Rais kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na EWURA, hususan juhudi zao katika kuhakikisha kuwa nishati ya jotoardhi inatumiwa ipasavyo kama chanzo cha nishati mbadala.
Kongamano hilo linaangazia teknolojia na fursa zinazopatikana katika sekta ya jotoardhi, ambapo wataalam kutoka ndani na nje ya nchi wanashirikiana kwa lengo la kuendeleza nishati endelevu nchini Tanzania.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED