WAKALA bora, Mino Raiola, na ulimwengu wa uhamisho wa wachezaji wa soka ulikuwa unaenda naye sambamba.
Raiola pengine alikuwa wakala mashuhuri zaidi kuliko wote, mwenye sifa ya kutisha ya kufanya mazungumzo ya juu zaidi kwa ajili yake na wateja wake.
Wasifu wake ulikosolewa na makocha wawili tu maarufu, Sir Alex Ferguson na Pep Guardiola.
Lakini kifo chake mwaka 2022 kilitarajiwa kuangusha himaya ya uhamisho ambayo Raiola alikuwa ameijenga kwa miaka mingi.
Binamu yake, Enzo anashiriki kumbukumbu yake anayemtaja kama "onesho la mtu mmoja" na anaelezea jinsi urithi wa Mino unavyoendelea.
Kujijenga upya katikati ya huzuni
"Kifo chake hakikutarajiwa kabisa," anasema Enzo Raiola katika mahojiao na BBC Sport.
"Hata alipokuwa mgonjwa, umakini wetu wote ulikuwa kumsaidia kupata nafuu.
"Hakuna kitu kilikuwa mahali, na hatukufikiria tungehitaji kupanga upya kila kitu huku tukiwa na huzuni - ilikuwa ngumu sana."
Mino alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 54 huko Milan Aprili 2022, na alipata heshima na rambirambi nyingi kutoka ulimwenguni kote.
Mshambulizi wa Manchester City, Erling Haaland alimwita "wakala bora zaidi", fowadi wa Italia, Mario Balotelli alisema alikuwa "baba yangu wa pili" na Zlatan Ibrahimovic alisema "nililia sana hadi tone langu la mwisho.”
Lakini familia ya Raiola ililazimika kusonga mbele haraka au kuhatarisha kupoteza biashara ya Mino, ambayo ilianzishwa kwa uhamisho wa kwanza wa Pavel Nedved na Dennis Bergkamp na baadaye ikaonesha hatua kubwa kwa Haaland na Paul Pogba.
Hivyo ndivyo, vyombo vya habari vya kimataifa vilivutiwa na Raiola, kulikuwa na ripoti za uwongo za kifo chake alipokuwa bado anapigania uhai wake.
"Tulikuwa na wachezaji wetu na vyombo vya habari vikiuliza hali yake - wakati mawakala wengine katika makampuni pinzani walijaribu kuiba wachezaji wetu," anasema Enzo.
"Ilitubidi tujipange upya na kuitikia kila kitu. Wakati wote nilipokuwa nikienda hospitalini kwa dakika za mwisho za Mino nilikuwa na woga wa kumpoteza.
"Nilikuwa nae kwa miaka 15. Mino alikuwa msukumo, baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya siku 30. Alikuwa onesho la mtu mmoja. Lakini hatukuweza kuacha kazi yake ipotee na ilibidi tujenge upya himaya yake."
Kifo kilibadili mambo
Wakati baadhi ya wachezaji wakubwa waliungana na mshirika wa zamani wa Raiola wa kibiashara Rafaela Pimenta, wengine walienda na Enzo - pamoja na skauti aliyeaminika zaidi wa Mino, Jose Fortes Rodriguez - katika operesheni iliyojengwa upya iliyopewa jina la Team Raiola.
"Mino hangeruhusu mtu yeyote kumkanyaga," anakumbuka Enzo. "Angepigana katika mazungumzo, au hata kwenye ukumbi wa hoteli ili kupata chumba sahihi.
"Alikuwa na pande mbili tofauti kwa utu wake. Katika mahojiano na mazungumzo, alionekana kuwa na ushindani mkali.
"Bado nyuma ya pazia na wachezaji wake na washirika anaweza kuonesha hisia kubwa ya huruma na ubinadamu.
"Mimi na Jose tunapenda kuingia ulingoni kuwalinda wachezaji wetu pia, lakini bado hatujazungumza waziwazi kwenye vyombo vya habari."
Kuangalia kizazi kipya
Raiola alikuwa ameona orodha ndefu ya wateja ikija na kuondoka, baada ya kuhusika katika mikataba ya uhamisho wa Romelu Lukaku, Marcus Thuram, Matthijs de Ligt, Noussair Mazraoui na Denzel Dumfries.
Raiola alipoanza kutoka katika maisha duni kwenye biashara ya mgahawa wa familia ya pizza huko Haarlem, karibu na Amsterdam, Enzo aliingia kwenye soka akiwa anaendesha karakana ya magari ya familia karibu na mji wa Naples.
Hatimaye alijiunga na binamu yake katika soka wakati wa uhamisho wa Ibrahimovic mwaka 2006 kutoka Juventus kwenda Inter Milan, akimsaidia Raiola kumhamisha mteja wake kutoka kwa wababe wa Turin walioshuka daraja wakati wa kashfa ya upangaji matokeo.
Timu iliyobadilishwa umbo la Raiola pia inawakilisha baadhi ya vipaji vinavyoongoza katika Ligi Kuu England - ikiwa ni pamoja na Micky van de Ven wa Tottenham Hotspur, Ryan Gravenberch wa Liverpool na Justin Kluivert wa Bournemouth.
Ili kuendana na matarajio ya kizazi kipya, Team Raiola hutumia kampuni tofauti inayoendeshwa na mtoto wa Raiola, Mario ambayo inajishughulisha na uchanganuzi wa data, haki za vyombo vya habari, udhamini wa chapa, mitandao ya kijamii na mawasiliano.
"Tunataka tu wachezaji 11 wa juu katika soko letu kudumisha mwingiliano kama familia," anasema Enzo.
"Lakini lazima pia tusiwe bendi ya mtu mmoja kama iliyokuwa hapo awali.
"Tunapoenda kwa klabu kufanya mazungumzo, wana silaha na data - unapaswa tu kuangalia jinsi Brentford na Brighton wanavyofanya kazi. Data inatumika kuchunguza kizazi chetu kijacho, katika maeneo ambayo tuna maskauti wachache."
Rodriguez - skauti wa muda mrefu aliyegeuka wakala wa Raiola - anashiriki mawazo fulani juu ya wateja wake watatu wa Ligi Kuu England.
Micky van de Ven
"Raiola alinipigia simu na kusema 'nimeona mchezaji mzuri sana katika Daraja la Pili Uholanzi huko Volendam'. Nikasema 'Hiki si kiwango cha wachezaji tunachoangalia', lakini Mino alisisitiza niangalie.
"Nilikuwa nimesikia hadithi kuhusu Van de Ven. Nilimpigia simu Mino baada ya dakika 20. Ilinichukua muda mrefu kuona vya kutosha kuhusu kasi na ujasiri aliokuwa akicheza nao.
"Wakati huo, nilimwambia Mino 'Tunahitaji kumchukua mchezaji huyu'. Siku zote nilikuwa nikifikiria anaweza kucheza Ligi Kuu England kwani ana nguvu kiakili na kimwili."
Ryan Gravenberch
"Nilipomuona Ajax kwa mara ya kwanza nilipenda sana kipaji chake.
"Nilikuwa kama 'Wow, wow, wow'. Alipokuwa na umri wa miaka 14 au 15 niliendelea kumwambia anaweza kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani.
"Bado anahitaji kuimarika kwa sasa kwa sababu Ryan ni mmoja wa wachezaji wanaohitaji kujionesha zaidi, ni mstaarabu sana uwanjani."
Justin Kluivert
"Nilimwona alipokuwa mdogo na tayari katika kikosi cha kwanza cha Ajax. Kila mtu aliona kuwa ana kazi kubwa mbele yake. Alikuwa mtu mkubwa.
"Amecheza ligi zote bora Ulaya na yuko Bournemouth, akitengeneza mabao.
"Nina furaha sana kwa Justin kwamba anaweza kufanya hivi katika kiwango hiki cha Ligi Kuu, lakini amekuwa akifanya hivyo tangu akiwa kijana mdogo."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED