Mkurugenzi Nsimbo ataka elimu ya lishe iwafikie wananchi

By Neema Hussein , Nipashe
Published at 08:33 PM Oct 22 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi Mha. Stephano Kaliwa.
Picha:Mtandao
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi Mha. Stephano Kaliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi Mha. Stephano Kaliwa amewataka wakuu wa idara kuhakikisha wanaibeba ajenda ya lishe kwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu.

Kaliwa ameyasema hayo katika kikao cha utekelezaji wa afua za lishe ambapo katika kikao hicho alimsimamisha kila Mkuu wa idara kueleza mikakati yake kuhakikisha jamii inapata elimu juu ya masuala ya lishe.

Amesema elimu ya lishe isiishie shuleni bali elimu hiyo itolewe kila nyumba na vituo vya afya pamoja na kuanzisha bustani za mboga shuleni na nyumbani.

Nickson Yohanes ni Afisa lishe Halmashauri ya Nsimbo, amesema umasikini ni moja ya sababu inayochangia wananchi kutotimiza makundi ya vyakula vinavyotakiwa.

Kwa upande wao baadhi ya wakuu wa idara wamesema elimu ya lishe itolewa hadi kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya Virus vya Ukimwi.