Mwanamke akutwa ameuawa huko Madina, Msangani

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 08:50 PM Oct 22 2024
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya.
Picha:Mtandao
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya.

MTU mmoja jinsia ya kike amekutwa ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulikana katika eneo la Madina Kata ya Msangani Wilaya ya Kibaha.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya amesema mwili huo wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30 umeokotwa jana Oktoba 21 majira ya saa saba mchana.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini mtu huyo alikuwa anaelekea katika mashamba pori ya Madina kwa kutumia usafiri wa pikipiki ambayo haikutambuliwa usajili wake wala dereva.

Kaimu Kamanda Msuya ametoa wito kwa wananchi na madereva wa pikipiki kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiwe, viongozi wa Mitaa na polisi wanapokuwa na mashaka kwa baadhi ya watu Ili kuepusha madhara ambayo ya aweza kutokea.