FCS, LATRA CCC waanza mradi kutetea haki za watumiaji wa usafiri ardhini

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 08:07 PM Oct 22 2024
Viongozi wakuu wa Taasisi za FCS na LATRA CCC wakisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika sekta ya ya Usafirishaji Ardhini
Picha:Elizabeth Zaya
Viongozi wakuu wa Taasisi za FCS na LATRA CCC wakisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika sekta ya ya Usafirishaji Ardhini

FOUNDATION For Civil Society(FCS) kwa kushirikiana na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini(LATRA CCC) wamesaini makubaliano ya kushirikiana kufanya kazi katika mradi wa kulinda na kutetea haki za watumiaji wa huduma za usafiri ardhini.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam na kushirikisha viongozi wakuu wa pande hizo mbili.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la LATRA CCC Daud Daudi, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za usafiri ardhini wanapata zile zinazostahili na kwa ubora.

Daudi amesema mradi huo ni wa miaka mitatu hadi 2027 na unalenga kuboresha huduma za usafiri ardhini, na kwamba umeanzishwa baada ya kubaini kuwapo kwa uhitaji wa elimu kwa umma kuhusu matumizi ya mifumo na miundombinu ya barabara.

“Ipo Sera ya Taifa ya Usafirishaji nchini ya mwaka 2003 ambayo kupitia Wizara ya Uchukuzi tupo katika mchakato wa kuiboresha, ili itupe nafsi  nzuri ya , kupenyeza maoni wa watumiaji,"amesema Daudi.

Amesema baraza hilo limekuwa likifanya kazi na wasafirishaji katika sekta hii ya ardhini, hivyo tunaamini kwamba, hata viwango vya nauli vitalingana nathamani ya huduma.

"Kwamba uwiano wa nauli zinazotozwa utalingana na thamani ya huduma, zikitolewa kwa ubora, kwa wakati husika na hali halisi ya maisha ya Watanzania,"amesema Daudi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, amesema mradi huo na LATRA CCC umekuja, ili kuimarisha mifumo na huduma ya usafiri ardhini nchini na kufanikisha maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.

"Na ndio maana tunasema jambo la kwanza ni lazima wananchi wapate huduma bora naka wakati na iendane na thamani ya fedha au nauli inayotozwa, kwa hiyo kwenye mradi huu pamoja na mambo mengine, lakini hilo nalo tutalizingatia,"amesema Ruteng