Singida watenga hekta 6,000 za ardhi kwa ajili ujenzi viwanda

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 05:33 PM Oct 23 2024
Singida watenga hekta 6,000 za ardhi kwa ajili ujenzi viwanda
Picha: Thobias Mwanakatwe
Singida watenga hekta 6,000 za ardhi kwa ajili ujenzi viwanda

MKOA wa Singida umetenga hekta 6,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambapo kwa sasa mkoa una kiwanda kikubwa kimoja vya kati 10, vidogo 309 na vidogo kabisa vipo 1,483.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, alimweleza hayo jana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Jerry Silaa, ambaye yupo kwenye ziara ya siku tano mkoani hapa kukagua miradi ya maendeleo.

"Kumekuwa na mwamko wa kujenga viwanda katika Mkoa wa Singida, hivi sasa kuna viwanda vitatu vikubwa ambavyo vimejengwa na vitazinduliwa hivi karibuni ambavyo ni kiwanda cha mafuta ya kula ya alizeti, kiwanda cha Sabuni za mche na kiwanda cha juisi,"alisema Dendego.

Kuhusu umeme, alisema hivi sasa vijijji vyote 441 vya Mkoa wa Singida vimeshafikishiwa huduma ya umeme na hatua inayofuata umeme umeanza kupelekwa kwenye vitongoji lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme.