Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC) umesisitiza uhitaji wa serikali kuweka utaratibu mathubuti wa usimamizi na ufuatiliaji wa uhai wa majengo hasa ya umma na biashara yanayo jumuisha idadi kubwa ya watu ili kuepuka athari zilizotokea jengo la Kariakoo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Ole Ngurumwa, amesema umefika wakati kwa mamlaka mbalimbali za serikali zinazohusika na usimamizi wa vibali kufanya ufuatiliaji kwenye majengo hayo.
"Uhitaji wa maboresho ya sheria inayosimamia majanga ili kuwe na kamati za kudumu zitakazokuja na suluhu za muda mrefu kutatua majanga na kuondokana na muundo wa kuwa na kamati zinazokutana baada ya matukio," amesema
Ameongeza kuwa, Tanzania kuna sheria ambayo inasimamia majanga ambayo ilitungwa mwaka 2015 na unaendelea kufanyiwa maboresho mara kwa mara.
Olengurumwa amesema suala la majanga ni endelevu hivyo wanapendekeza kuwe na kamati ya majanga ya kudumu iwe ya kufuatilia, kujua na kubatili majanga nchini na kutoa elimu kwa wananchi.
Akizungumzia kuhusu changamoto mbalimbali ambazo zinejitokeza kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa amesema Novemba 20, wanatarajia kuanza kampeni hivyo asilimia 99 serikali ya mtaa inaunganisha jamii na wananchi.
"Mtandao huu umehimiza uhitaji wa kufanyika kwa Uchaguzi huru na wa haki kupitia mifumo sahihi ya usimamizi wa uchaguzi," amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED