MOI yagawa zawadi za sikukuu kwa watumishi wake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:32 PM Dec 24 2024
MOI yagawa zawadi za sikukuu kwa watumishi wake.
Picha:Mpigapicha Wetu
MOI yagawa zawadi za sikukuu kwa watumishi wake.

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas kwa watumishi wake 1052, ili kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wagonjwa .

Zawadi hizo ambazo ni Kilo 15 za mchele, lita 2 za mafuta ya kupikia na vinywaji zenye thamani ya shilingi  50,000 zimekabidhiwa jana Jumatatu Desemba 23, 2024 kwa wawakilishi wa watumishi hao na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Dk. Mpoki Ulisubisya.

Akikabidhi zawadi hizo Dk. Mpoki alisema kuwa menejimenti ya MOI imewapa motisha watumishi wake ya mkono wa Sikukuu ya Krismas kwa kutambua mchango wao mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.

"Menejimenti ya MOI tumetoa zawadi na shukurani hizi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wenu mkubwa hususani wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, pia tunaomba msheherekee sikukuu kwa amani na furaha"- alisema Dk. Mpoki

Kwa upande wake, Mhudumu wa Afya wa MOI, Amina Makunga aliishukuru menejimenti ya MOI kwa kuwapatia zawadi hizo kwani ni inawapa morali na motisha ya kufanya kazi zaidi ya kutia huduma za matibabu kwa wagonjwa.