Watu 7 wafariki dunia ajali ya lori na costa Handeni

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:18 PM Dec 24 2024
Watu 7 wafariki dunia  ajali ya lori na costa  Handeni.
Picha:Mtandao
Watu 7 wafariki dunia ajali ya lori na costa Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando, amethibitidha kutokea kwa ajali siku ya leo eneo la Michungwani kwenye wilaya yake ya Handeni iliyosababisha vifo vya watu 7 na majeruhi 10, kupitia kurasa yake ya Instagram Msando ameandika.

“Leo asubuhi mida ya saa 12 imetokea ajali iliyohusisha Lori na Coaster. Ajali hiyo imetokea eneo la Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni. Watu 7 wamepoteza maisha na 10 wamejeruhiwa. Naendelea kuwasisitiza sana madereva kuwa makini na kuchukua tahadhari.

Ajali hii sababu ni uzembe wa dereva. Kwa sababu ya kujirudia rudia kwa uzembe nimemuelekeza OCD atakayekiuka sheria ya barabarani eneo la Handeni tutampandisha Mahakamani na kuomba adhabu ya kifungo.

Kwa ambao mmekuwa mkipiga simu kusaidiwa madereva wenu wakikiuka sheria za barabarani wala msisumbuke: hakuna msaada zaidi ya kukaa lock up kwa mujibu wa sheria na kupandishwa kizimbani. Ukifika kijiji cha Manga Wilaya ya Handeni ewe Dereva usipofuata sheria za usalama barabarani usitulaumu.

Ajali nyingi zinaepukika. Na abiria, acheni kukaa kimya wakati dereva anaendesha hovyo aidha shuka utarejeshewa nauli yako na toa taarifa kwa Jeshi la Polisi tudhibiti huu uzembe.