GGM yakabidhi polisi pikipiki 50

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:13 PM Oct 23 2024
GGM yakabidhi  polisi pikipiki 50
Picha: Mwandishi Wetu
GGM yakabidhi polisi pikipiki 50

MGODI wa dhahabu wa Geita (GGML) umekabidhi pikipiki 50 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya kuboresha usalama, kuimarisha utendaji kazi na kurahisisha harakati za polisi za kufuatilia wahalifu na kuibua matukio ya uhalifu kabla ya kusababisha madhara.

Pikipiki hizo zenye thamani ya Sh. milioni 175  zitagaiwa kwa askari polisi ngazi ya kata, ili wafanye kazi kwa ufanisi  na kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo kuanzia ngazi za chini. 

Akizungumza jana Oktoba 22,2024 wakati wa kukabidhi pikipiki hizo Makamu wa Rais Mwandamizi wa Anglogold Ashant Afrika,Terry Strong amesema pikipiki hizo zimetolewa, ili z kusaidia kulinda mali na kuimarisha ulinzi na usalama kwa mkoa wa Geita. 

Amesema kama kampuni ya uchimbaji lengo lao ni kuona jamii inayowazunguka inanufaika na shughuli zao na kwamba kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi na kuhakikisha wananchi wanakuwa salama. 

Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya Jeshi la Polisi Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, amesema lengo la kupeleka askari kuanzia ngazi ya kata ni ili waweze kukaniliana na matukio ya uhalifu kabla ya kuleta madhara ili waweze kuyadhibiti. 

1

Amesema Mkoa wa Geita ni miongoni mwa mkoa wenye matukio ya uhalifu yanayosababishwa na ujinga hususa pale wanaporubuniwa na waganga wa kienyeni hivyo kusababisha madhara kwa wananchi. 

“Elimu bado inahitajika nasema hivi kwakuwa wakati mwingine mganga wa kienyeji anamrubuni mtu ili upate utajiri baka mtoto mchanga huyo mpiga ramli chonganishi mwenyewe hana utajiri kuna haja ya polisi kata kuwatambua wanaofanya uhalifu wakiwemo hao wanaopiga ramli chonganishi nna kutoa elimu kuhusu masuala yanayohusu usalama wa jamii,”amesema Masauni. 

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela,  amesema ushirikiano wa sekta binafsi na umma ni muhimu katika kujenga taifa lenye usalama na utulivu. 

Aidha, amesema GGML imesaidia watanznaia wengi kupata ajiora hivyo kusaidia kukuza uchumi wa mkoa huo ambapo amesema katika uwajibikaji wa kampuni kwa jamii mgodi huo kila mwkaa hutoa Sh. bilioni 9.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Askari Polisi  Kadogo Venance askari amesema kwa kupata usafiri huo kutasaidia waweze kufika kwenye tukio kwa wakati na kudhibiti uhalifu kabla ya kusababisha madhara.

2