Kura za kushangaza tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:22 AM Dec 23 2024
Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fifa wa Mwaka 2024, Vinicius Junior (kushoto), akipongezwa na rais wa Shirikisho hilo la Soka duniani, Gianni Infantino, Desemba 17, mwaka huu.
PICHA: MTANDAO
Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fifa wa Mwaka 2024, Vinicius Junior (kushoto), akipongezwa na rais wa Shirikisho hilo la Soka duniani, Gianni Infantino, Desemba 17, mwaka huu.

HUENDA ikakosa uzuri na hadhi ya Ballon d'Or, lakini tuzo ya FIFA ya mwanasoka bora wa mwaka bado inapamba vichwa vya habari kila mwaka.

Hafla hiyo ilifanyika Jumanne ya Desemba 18 ambapo manahodha na makocha wa timu za taifa ndio wapigaji wa kura, huku Vinicius Junior akiitwaa baada ya kuikosa ile ya Ballon d'Or.

Raia huyo wa Brazil aliwashinda bingwa wa Ballon d'Or, Rodri pamoja na Jude Bellingham, Dani Carvajal, Lamine Yamal na wengine. 

Ilikuwa tuzo yake ya kwanza kwa winga huyo wa Real Madrid, ambaye alipigiwa kura na mchanganyiko wa manahodha na makocha wa timu za taifa, waandishi wa habari na mashabiki.

Wakati Vinicius alikuwa mshindi aliyestahili wa Tuzo Kuu ya FIFA katika soka la wanaume, kulikuwa na kura ambazo ziliibua mshangao.

Harry Kane amkataa Bellingham

Upigaji kura wa tuzo za soka mara nyingi huwaona wachezaji wenzao wakishikamana na kusaidiana. Lakini nahodha wa Timu ya Taifa ya England na fowadi wa Bayern Munich, Harry Kane, aliamua kutomtunuku Muingereza mwenzake, Bellingham katika kura yake.

Kane alimweka Bellingham katika nafasi ya pili, huku Rodri akishika nafasi ya kwanza na mshindi Vinicius akishika nafasi ya tatu.

Bellingham aliingia kwenye tuzo hizo baada ya mwaka wa kustaajabisha na Real Madrid. Alishinda LaLiga na Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na 'Los Blancos' hao, huku pia akiisaidia England kufika fainali ya Euro 2024.

Vyombo vya habari vya Argentina vyampuuza Messi

Lionel Messi hatakiwi kufanya mambo mengi sana ili aonekane kwenye orodha fupi ya tuzo kuu za soka siku hizi. Messi tayari ameshinda mara nane tuzo ya Ballon d'Or, alishinda Copa America 2024, lakini bila shaka hakuwa miongoni mwa wanasoka 11 bora zaidi wa kiume duniani mwaka huu.

Mwandishi wa habari wa Argentina, Claudio Mauri yeye hakumpigia kura Messi, badala yake alimchagua Rodri, Lamine Yamal na Toni Kroos.

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, alimpigia kura Messi, na kumweka katika nafasi ya kwanza. Messi mwenyewe alimpigia kura Yamal.

Erling Haaland akataliwa Norway

Jina la Erling Haaland lilikuwa moja wapo ya chaguo maarufu zaidi kati ya wapigakura, akimaliza katika nafasi ya nane. 

Fowadi huyo wa Manchester City alishinda Ligi Kuu England na kumaliza kama mfungaji bora msimu wa 2023/24, lakini alizidiwa na mwenzake Rodri.

Ni wazi nahodha wa Norway na Arsenal, Martin Odegaard alihisi vivyo hivyo. Alimweka mchezaji mwenzake wa kimataifa katika nafasi ya tatu, akiwaweka Rodri na Vinicius mbele yake, huku kocha wa Norway, Stale Solbakken akimweka Haaland nafasi ya pili.

Haaland pia alinyimwa nafasi ya kwanza na mwakilishi wa vyombo vya habari vya Norway, Morten Pedersen, ambaye, kama Odegaard, alimchagua katika nafasi ya tatu.

Makocha wa timu za taifa

Makocha wa timu za taifa hutazama soka kwa miezi michache tu ya mwaka kulingana na upigaji kura. Mabosi wengi wa timu ya taifa walipanga viwango vitatu vya juu vya ajabu, zaidi ya kocha wa Uswisi, Murat Yakin.

Wachezaji watatu bora kati ya Florian Wirtz (wa kwanza), Federico Valverde (wa pili) na Lamine Yamal (wa tatu) watawashangaza wachache, huku Rodri na Vinicius wote wakipuuzwa.

Kocha wa Ujerumani, Julian Nagelsmann bila mshangao aliwateua Wajerumani Wirtz na Toni Kroos, akiwaacha Vinicius, huku Kocha wa Ubelgiji, Domenico Tedesco akiwateua Yamal, Wirtz na Haaland kama watatu anaowapendelea zaidi.