RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa IGP, Said Mwema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN), akichukua nafasi ya Hab Mkwizu ambaye amemaliza muda wake.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa Novemba 27,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, imeeleza Rais Samia amemteua David Mwakyusa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Pia amemteua Mhandisi Mussa Natty kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), akichukua nafasi ya Joseph Haule ambaye amemaliza muda wake.
Mwema amewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania tangu mwaka 2006 na anakumbukwa kwa kuanzisha polisi jamii.
Aidha,Prof.Mwakyusa amewahi kuwa Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi tangu mwaka 2005 hadi 2010 katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Mhandisi Natty, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Babati akitokea Manispaa ya Kinondoni.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED