RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa pongezi kwa kundi la ‘The Ramadhani Brothers’ kuandika historia ya kuwa Watanzania wa kwanza kushinda mashindano makubwa ya kusaka vipaji American Got Talents: Fantasy League.
Katika ukurasa wake binafsi wa Instagram, Rais Samia ameandika: “Pongezi kwa vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League. Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine.
Kundi hilo linaloundwa na ndugu wawili (Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu), ambao wametangazwa washindi kwa umahiri wao katika sarakasi (Acrobatics) usiku wa jana Jumatatu, na hivyo kuondoka na kibunda cha zaidi ya Tsh Milioni 600.
“Hatimaye safari yetu imefikia hapa, tuna furaha kuwa washindi wa AGT Fantasy League duniani, asante kwa mashabiki wote na washiriki wenzetu” - wameandika Ramadhani Brothers baada ya ushindi huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED