KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi, Amos Makalla amesema mabadaliko katika mfumo wa uchaguzi ikiwemo mabadiliko katika tume ya uchaguzi tayari yamefanyika na kwamba suala la uchaguzi halizuiliki.
Akizungumza katika mahojiano maalum na chombo kimoja cha habari nchini, Makalla amesema uchaguzi ni suala la kisheria na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuzuia sheria kutekelezwa.
“Zipo ajenda za siri nyuma ya no reforms no election lakini mabadiliko yakwisha kufanyika, hawa (CHADEMA) hawana hela ya kufanya uchaguzi ,muda umebaki mdogo na hawajajiandaa” amesema Makalla.
“Wanawahadaa watu kwamba watazuia uchaguzi hawawezi kuzuia uchaguzi, na inajulikana kwa sababu sheria zipo, ameseama wataishurutisha serikali sasa huwezi kuishurutisha serikali” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED