KATIKA kutambua mchango mkubwa wa uwekezaji , utoaji huduma na ubunifu, kampuni ya huduma za simu ya Yas Tanzania leo imetunukiwa tuzo tatu katika sekta ya Tehama.
Katika tuzo hizo za Tehama zilizotolewa jijini Arusha, Yas imeshinda katika kipengele cha Huduma bora za Intaneti (Best Internet Service Provider).
Tuzo nyingine waliyoishinda ni tuzo ya Kampuni Bora ya Mawasiliano Tanzania (Best Mobile Network Provider) na tuzo ya Mtumiaji Bora wa Tehama na Manufaa kwa Jamii.
Tuzo zimetolewa kwenye ukumbi wa Gran Melia jijini Arusha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED