JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Kisangeneni Kata ya Kahe wilayani Moshi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanae wa kumlea mwenye umri wa miaka 13.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa alisema baba huyo mlezi anadaiwa alikuwa akifanya nae mapenzi kwa nyakati tofauti tangu akiwa darasa la tatu huku akimtishia kumuua ikiwa angetoa taarifa hizo.
Kamanda alisema hali hiyo imepelekea mwanafunzi huyo kushindwa kuanza masomo yake ya sekondari ya kidato cha kwanza mwaka 2025 ambapo inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa akimtishia kumuua mwanafunzi huyo iwapo atatoa siri hiyo.
Kamanda alisema baada ya mama mzazi wa binti huyo kubaini tukio hilo, mwezi Oktoba mwaka jana alimsafirisha binti huyo kwenda kwa baba yake mzazi jijini Dar es salaam bila kutoa taarifa kituo chochote cha polisi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED