Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa msaada wa kijamii wa fedha taslim, vifaa tiba pamoja na vifaa mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu na watoto yatima (KIDEP) kilichopo Moshi , Mkoani Kilimanjaro.
Vifaa hivyo ni pamoja na mchele kg 100, maharake kg 50 , sabuni za kufulia viroba viwili, mafuta ya kupikia lita 20, peni , penseli, mataulo, dazeni za counter books, dazeni za daftari ndogo, mafaili, dagaa ndoo kubwa mbili, maharage kilo 50 crashing za kusafishia choo na za kuoshea viatu.
Akizungumza kwa niaba ya Mfuko, Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Linda Balama alisema Mfuko umeguswa na uhitaji wa watoto hao na hivyo kuandaa vitu hivyo kufanya watoto hao wafurahi kama watoto wengine.
Aidha, Muanzilishi wa kituo hicho Diomedi Msindi aliwaeleza watumishi hao kuwa kituo kinapitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ada za watoto, chakula, mahitaji ya shule, kodi ya nyumba wanayoishi, malipo ya maji na umeme pamoja na vitu vingine. Alishukuru sana watu wa PSSSF kwa msaada huo ambao alisema kwa kiasi kikubwa itawasaidia watoto.
Kundi hilo la wakimbiaji 100 kutoka PSSSF mikoa mbalimbali ambao wako Moshi, mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kukimbia riadha ya Kili Marathon hapo kesho, walipata nafasi ya kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED