Malela Herbalist Clinic kuandaa tamthilia ya African Spirit

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 04:40 AM Feb 16 2025
Mkurugenzi Mtendaji  wa Mkali  Malela Herbalist Clinic, Riziki Mkali.
Picha: Iman Nathaniel
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkali Malela Herbalist Clinic, Riziki Mkali.

Kampuni ya Malela Herbalist Clinic Limited imetangaza kuja na maandalizi ya tamthilia kubwa na ya kipekee itakayojulikana kama “African Spirit.

Tamthilia hyo inalenga kuibua na kuonyesha kwa undani historia, mila, na matukio muhimu ambayo yalikuwa hayajapewa thamani stahiki katika bara la Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji  wa Mkali  Malela Herbalist Clinic, Riziki Mkali ,  amesema kuwa  ,Tamthilia ya “African Spirit” si tu itakuwa burudani ya hali ya juu, bali pia italeta  hamasa
ya kuamsha fikra, jicho la kuonyesha mila zetu, na chombo cha kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kuthamini urithi wa Afrika. 

"Tunajivunia sana kuanzisha mradi huu wa Tamthilia ya Afriacan Spirit, tunamaamini itakuwa chachu ya mabadiliko , si tu kutangaza mila ba tamaduni zetu bali kwa kuelimisha na kuunganisha jamii ya Afrika na ulimwengu mzima.

Aidha Kupitia matukio na visa vya kusisimua na maudhui yanayogusa jamii, Tamthilia hii italenga kusambaza ujumbe huu Afrika na ulimwengu mzima ili
kuona uzuri wa mila zetu za Kiafrika ambazo kwa muda mrefu zimeachwa nyuma au kupuuzwa.

Amesema Tamthilia hii itakuwa na malengo mbalimbali ikiwamo, kukuza Utambulisho wa Kiafrika, Elimu na Uhifadhi wa Mila na kuunganisha jamii .

Kwa upande wa muandaajinwa Tamthilia hiyo, Octavian Vitus, amesema kuwa maandalizi ni mazuri ambayo amabapo iatalenga kuondoa imani potofu katika jamii.