Mabadiliko ya tabianchi inavyoweza kuathiri Dira Maendeleo Taifa ijayo

By Flavian Jeremiah , Nipashe
Published at 11:26 AM Mar 26 2024
Pori linaloonekana limeathrika na mabadiliko ya tabianchi wialayani Longido.
Picha: Mtandao
Pori linaloonekana limeathrika na mabadiliko ya tabianchi wialayani Longido.

TUNAKUMBUKA serikali nchini ilitengeneza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, katika kuongoza harakati ya maendeleo ya uchumi na jamii kwa taifa.

Hiyo hata ikawa msaada, kuiwezesha nchi kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati na kuondokana na idadi kubwa ya umasikini uliokithiri kwa Watanzania. 

Uboreshaji wa hali ya maisha ya Watanzania, ni kujenga utawala bora na kuhakikisha kunakuwapo mazingira ya amani, usalama na umoja, kutengeneza jamii iliyoelimika vyema, kukijenga uchumi imara nchini.  

Ni vitu vilivyopewa kipaumbele katika Dira Maendeleo ya Taifa. Pamoja na jitihada mbalimabli zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi na mashirika binafisi ya ndani na nje ya nchi, kumekuwapo athari kubwa zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi katika uchumi kama. 

Hapo unaingia mfano wa sekta ya kilimo kinachotegemewa na idadi kubwa ya Watanzania, wastani asilimia 75 na mifumo ya biashara ya kimataifa. Hata hivyo, kama nchi tunakwazwa kufikia baadhi ya malengo katika mikakati ya Dira ya Maendeleo 2025.  

Inaangukiwa na sababu kama, milipuko wa janga la maradhi Uviko 19, athari za mabadiliko ya tabianchi, ambazo zimekuwa tishio kubwa kwa uchumi wa taifa. 

Mabadiliko hayo ya tabianchi, yameleta athari kubwa katika sekta kubwa na muhimu zinazotegemewa na serikali, pamoja na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

 Hivyo zimekuwa miongoni mwa vikwazo vinavyokwamisha maendeleo, pamoja na jitihada zinzochukuliwa kupunguza athari tajwa za mabadiliko ya tabianchi. 

 Sasa, katika kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050, kama nchi pamoja tuna wajibu wa kuhakikisha tunaongeza nguvu katika kupambana na janga hilo, ili kupunguza athari tajwa, kwani kufikia mwaka 2050 inakadiriwa sekta za kilimo, uvuvi pamoja ma ufugaji zitaathiriwa zaidi, hata kupunguza shughuli hizo kwa asilimia 2.8. 

 Ni athari zinazochangia katika upatikanaji ajira, pia chakula cha kutosha, viwanda na biashara navyo havibaki salama.

 Kuguswa huko kwa sekta muhimu, kinamana katika uwanda wa pato la taifa, matarajio ni kupungua kwa chini ya asilimia moja katika safari kusonga mwaka 2030 kuchumi. Hivyo ni jambo linalotujengea wajibu wa kila 

mmoja kuendelea kupambana kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwani huathri kila mtu.

 Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, tunajua iko mahali hapo kushirikiana na taasisi na mashirika ya ndani na kimataifa zikichukua tahadhari na kuunda mikakati, pia sera wezeshi zinazopunguza vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi na kujenga uwezo wa kuendelea kukabiliana na athari zake.

 Hizo ni pamoja na kuendelea na matumizi ya nishati safi na ufanisi kama vile umeme na gesi asilia, matumizi ya mkaa mbadala na vyanzo vinginevyo ambavyo ni nafuu kwa watu, vikiendana na uhalisia wa uchumi wa Watanzania, ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kama vyanzo vya msingi vya nishati.

 Ipo nafasi inayotajwa ya kuendelea kujenga miundombinu inayo weza kuimiri athari ya mabadiliko ya tabianchi, hasa mvua ambazo zimekuwa zikichangia mafuriko na uharibifu wa miundombinu, hata kuwajibisha serikali kujenga madaraja imara.

 Jitihada nyinginezo ni za kutolewa elimu ya kutosha kwa watu juu ya mabadiliko ya tabianchi, teknolojia za kupunguza vyanzo vya uchafuzi mazingira (vinavyosababisha kutokea kwa mabadiliko ya tabianchi), kusimamia sheria na sera za mazingira.

 Dhamira hapo inatajwa kuwa ni kuhakiksha hatua za utunzaji mazingira kupunguza mabadiliko ya tabianchi zinazingatiwa katika kila sekta za uchumi, kuliwezesha taifa kufikia malengo yatakayopangwa katika Dira ya Taifa ya 2025-2050.