MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema kwa sasa ni zamu ya mchezo wa raidha kuamka na kpanda juu baada ya soka.
Akizungumza kwenye mbio za Kimataifa za 'Tigo- Zanter Marathon 2024' zilizofanyika leo asubuhi Zanzibar, Makamu wa pili wa Rais Abdulla, amesema mchezo wa soka Zanzibar umepiga hatua ambapo kumekuwa na timu nyingi na vijana wengi wanashiriki hivyo lazima na riadha nao uinuke visiwani humo.
"Nawapongeza waandaaji wa mbio hizi, ni wakati sasa kwa mchezo huu wa riadha kuinula huku Zanzibar kama ilivyo soka," amesema.
Makamu wa Pili wa Rais amemuwakilishi Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi na kushiriki matembezi ya kilometa tano.
Mbio hizo zinazofanyika kwa msimu wa nne mfululizo zilishirikisha mami ya wakimbiaji kutoka Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Awali akizungumzia mbio hizo, Mkuu wa biashara wa Tigo- Zantel, Isaack Nchunda, amesema wanaamini mbio hizo zimeongeza chachu ya ukuaji wa uchumi visiwani humo.
"Tunaamini mbio hizi zinatupa jukwaa bora zaidi la kutangaza utalii wa Zanzibar, kukuza vipaji vya wanariadha, kuimarisha afya, na kuchangia katika kuchagiza uchumi wa bluuhapa visiwani hapa," amesema Nchunda.
Aidha, amesema dhamira ya kampuni hiyo ni kuendelea kuleta mabadiiko chanya kwenye jamii kwa kuwekeza kwenye miradi na matukio yanayogusa maisha ya wananchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED