KILELE cha Mashindano ya Ubunifu wa Akili Bandia Afrika yamepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 13 hadi 17, mwaka huu jijini, Dar es Salaam.
Mashindano hayo yatashirikisha vijana wabunifu ambao watatengeneza maroboti yatakayotumika kufanya kazi mbalimbali.
Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mohamed Abdullah, alisema lengo la mashindano hayo ni kutaka vijana kwenda na teknolojia za kisasa lakini pia kuhimiza matumizi ya TEHAMA.
Abdullah alisema vijana wote wenye nia nzuri ya kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kufanya hivyo ili kujiongezea ujuzi katika masuala ya teknolojia mpya ambayo inahimizwa matumizi ya TEHAMA.
Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha vijana wanabadilika katika matumizi ya TEHAMA na kuongeza hawataki kuona vijana wanabaki nyuma.
Aliongeza siku hiyo kutakiwa na roboti za aina mbalimbali zitakazoonyeshwa kwa watu watakaoshiriki katika mashindano hayo huku Dola za Marekani 100,000 zimetolewa kwa ajili ya washindi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED