Chereko Rufiji, mbaazi sasa zao la mnada, bei yaruka 300/- hadi 1,753

By Yasmine Protace , Nipashe
Published at 10:20 AM Sep 20 2024
Meneja wa CORRECU Mkoa wa Pwani, Hamis Mantawela, akipokea bei ya mnada wa mbaazi uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka kwa wanunuzi.
PICHA: YASMINE PROTACE.
Meneja wa CORRECU Mkoa wa Pwani, Hamis Mantawela, akipokea bei ya mnada wa mbaazi uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka kwa wanunuzi.

MBAAZI ni zao, linalolimwa maeneo mbalimbali ya mikoa hapa nchini, lakini wengi walilima zao hilo kama kitoweo.

Kutokana na kuona zao hilo kama ni kitoweo, hawakulitilia mkazo kwa kulilima kwa wingi, kutokana na sababu hawakujua kama linaweza baadae kuwa mkombozi wao. 

Inaelezwa kuwa miaka ya nyuma, waliolima mbaazi waliuza kilo moja kwa shilingi 200 na uuzaji huo uliwafanya walimaji washindwe kulima zao hilo kwa wingi, wakibaki katika kuamua kulima kidogo ngazi ya kufanya kitoweo. 

Hata hivyo, baada ya kuwapo mfumo wa kuuza mazao ya wakulima kwa kwa njia ya mtandao, ambao mfumo huo umeandaliwa na serikali umekuwa ukifanyika kwa njia ya minada ambao wakulima hukusanya mazao yao kupitia vyama vya msingi na kisha mazao hayo kuuzwa kwa njia ya mnada. 

Hivi karibuni Meneja wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU), Hamis Mantawela linakuja zao la, anasema baada ya kwisha kwa uuzwaji zao la ufuta katika mkoa wa Pwani, sasa ni msimu wa kuuza mbaazi na kisha korosho. 

Anasema, hata kama wakulima watakuwa wamelima mbaazi kidogo, anawasihi waikusanye katika maghala yao, ili ziuzwe katika mnada wanufaike na kujiongezea kipato. 

" Tunajua mnaweza mkawa na mbaazi chache (kidogo) majumbani, nyie leteni katika mnada, huku bei itakuwa nzuri kuliko kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo," anasema. 

 Anafafanua kuwa mkoa wa Pwani, zaidi ya tani 100 wamekusanya na matarajio ya mnada wa pili wamefanikiwa kuuza kilo moja ya mbaazi kwa shilingi 1,753. 

 Mantawela anasema ni jukumu la wakulima kuongeza uzalisha zao la mbaazi, ili waweze kunufaika nalo na katika miaka ya nyuma, mbaazi iliuzwa kilo moja shilingi 200 hadi 300, lakini mnada umefanyika na kuuzwa kwa bei hiyo mpya, shilingi 1753 kwa kilo moja. 

Anasema kutokana na hali hiyo, wakulima wanatakiwa kuboresha kilimo chao, ili bei kuwezesha bei inaongezeka maradufu. 

" Wakulima wanatakiwa kuboresha mashamba yao, ikiwamo kuboresha kilimo chao, ili waweze kunufaika kwa kuuza kwa bei kubwa,” Mantawela anasema. 

Anarejea katika mkoa wa Pwani, wakulima wake wamechelewa katika kilimo kukifanikisha kilimo cha mbaazi. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) cha Ikwiriri AMCOS, Kassim Mpwele, anaeleza wanafurahi kilimo cha mbaazi kuingizwa katika biashara hiyo tajwa. 

Kassim ambaye pia ni mwakikishi wa wakulima wa Kibiti CORRECU mkoani Pwani, akatumia nafasi hiyo kuwaahidi wakulima kuweka mbegu bora za mbaazi, ili mwakani wanufaike zaidi. 

Anaeleza, zamani walikuwa wakilima mbaazi na kukifanya kitoweo pekee, saa anasifu mageuzi ya sasa kwa mkulima biashara ya mbaazi imekuwa nzuri zaidi.

 SAUTI YA WAKULIMA

Amina Jumanne, Mkulima wa Mbaazi Kibiti, anaeleza kuishukuru serikali kuliona zao la mbaazi, nalo liuzwe kwa njia ya mnada, akitaka

 elimu itolewe zaidi kwa wakulima wa mbaazi wanufaike na mageuzi hayo. 

Bakari Juma, mkulima wa ufuta na korosho anasema watu wamekuwa wakilima mbaazi majumbani ikiwa ni kitoweo, lakini mageuzi hayo mapya, sasa zao hilo likiingizwa katika mnada wa mauzo ya mazao, imani yake ni kwamba mwaka ujao wakulima wake wataongezeka, hata uzalishaji nao kutanuka . 

" Zamani watu walielekeza nguvu katika ufuta na korosho, leo tena kuna  zao la mbaazi, hivyo inatakiwa elimu itolewe, mwakani walime mbaazi kwa wingi," anasema. 

Shaban Juma mkazi wa Kibiti pia mkulima wa ufuta, korosho na mbaazi, ana mtazamo wake kutaka elimu itolewe kwa wananchi waweze kunufaika na zao hilo. 

Anasema kutokana na watu wengi kulima mbaazi kama kitoweo, sasa watalima kwa wingi kama zao la biashara.